Translate

Sunday 6 May 2012

Matibabu ya Kienyeji na Matumizi ya Miti Shamba

Matumizi ya miti shamba na tiba za kienyeji yameongezeka sana. Kwa kawaida, watu hutumia tiba hizi kwa magonjwa ya kudumu ambayo dawa za kawaida zimeshindwa kutibu. Watu pia huzitumia kwa ajili ya kuboresha afya yao kwa jumla.
Tiba za kienyeji na miti shamba hutibu mwili mzima badala ya ugonjwa fulani au dalili za ugonjwa fulani. Wakati mwingine, zinatibu kuumwa na maumivu ambayo dawa za kuandikiwa na daktari haziwezi. Kwa mfano, kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo na maumivu wakati wa hedhi.Tahadhari – Kuchanganya dawa za kienyeji na dawa za kuandikiwa na daktari kunaweza leta athari usizotarajia. Kabla hujaanza kutumia tiba yoyote ya kienyeji, ongea na daktari.

No comments:

Post a Comment